Maswali ya Mara kwa Mara (FAQ)
Majibu ya haraka kuhusu uchaguzi wa tiles, wishlist, delivery na mawasiliano na timu yetu.
Ni tile gani zinafaa kwa chooni?
Kwa chooni, chagua floor tiles zenye anti-slip/matte finish ili kupunguza kuteleza. Ukutani unaweza kutumia polished au matte kulingana na design.
Tiles za kutereza zinafaa chooni?
Hazipendekezwi kwa sakafu ya chooni. Chagua tiles zenye rough au matte finish (anti-slip) hasa maeneo yanayolowa maji kila siku.
Ninathibitishaje bei na stock?
Tupigie au tuandikie WhatsApp 0716002790. Tutakuelekeza duka lenye tile unayotaka na kukusaidia kuhusu delivery.
Nitanunua vipi kwa usahihi idadi ya box?
Tumia tile calculator kwenye app: weka urefu na upana wa chumba, app inakukokokotoa box zinazohitajika.
Ninaweza kuchukua wapi oda yangu?
Unaweza kuchukua katika maduka/godowns ya mshirika: Magomeni, Kwapweza, Kwawazee, Gulioni, Mpendae, Darajabovu, Kisauni n.k.
Je, delivery ipo?
Ndio, delivery inaweza kupangwa kwa maelewano. Gharama ya usafiri hutegemea eneo la mteja.
Nifanye nini tile ikifika imeharibika?
Toa taarifa haraka kwa simu/WhatsApp 0716002790 ukiambatanisha picha na namba ya oda ili timu ikusaidie mapema.
Ninawezaje kuhifadhi tile ninayoipenda?
Bonyeza alama ya nyota kwenye tile. Tile itabaki kwenye wishlist ya simu yako na unaweza kuishare nasi WhatsApp.